Unataka Watu Wakusaidie? Hii Ndiyo Siri Wanayokuficha…

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Mara nyingi tumefundishwa maneno haya: “Hakikisha unazungukwa na watu ambao siku ukiwa na shida ya milioni moja, ukipiga simu moja tu uwe umeipata.”
Ni kweli kabisa, kuwa na mtandao wa watu wenye msaada ni jambo muhimu. Lakini kuna jambo ambalo hatufundishwi mara nyingi — kuwa mtu wa thamani kwa hao watu tunaowazunguka.

Kwa nini hili ni muhimu? Kwa sababu rafiki zako, ndugu zako au watu wa karibu watakupa msaada kulingana na thamani waliyoiona ndani yako. Ukiwa mtu wa kuaminika, mwenye kusaidia, mwenye heshima, na mwenye kutunza uhusiano, hakuna atakayeona tabu kukusaidia ukiwa kwenye changamoto kubwa.

Watu wengi wanajua kutafuta msaada, wachache wanajua kuwa msaada

Ukiangalia vizuri, kila mtu anapenda kusaidiwa, lakini wachache sana hujiuliza: “Mimi mwenyewe ni msaada wa nani?”
👉 Je, watu wanaweza kukupigia simu saa mbili usiku na kuwa na uhakika utawasaidia?
👉 Je, kuna mtu anayeweza kukuona kama chaguo la kwanza anapohitaji msaada mkubwa?

Kama jibu ni hapana, basi bado safari ya kujenga thamani haijakamilika.

SOMA: Kitabu: Usiishie Njiani, Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako

Usijenge tu mtandao wa kukusaidia

Kosa kubwa tunalofanya ni kutafuta watu wa kutusaidia sisi peke yetu. Lakini ukweli ni kwamba uhusiano wowote una afya unajengwa kwa ushirikiano na thamani ya pande zote mbili.

Kwa hiyo badala ya kuuliza “nitapata nini kwa fulani?” jiulize pia:

  • “Fulani anapata nini kwa mimi kuwa kwenye maisha yake?”
  • “Watu wakinitaja jina, wananihusisha na nini?”

Thamani yako inazidi pesa

Watu wengi hufikiri thamani inahusiana na mali pekee. Ukweli ni kwamba, thamani ya kweli ni zaidi ya pesa:

  • Ni heshima unayowapa wengine.
  • Ni uaminifu unaojijengea.
  • Ni msaada unaotoa hata bila kuulizwa.
  • Ni mawazo mazuri unayochangia.
  • Ni uwepo wako unaotoa faraja kwa wengine.

Wakati mwingine hata usipokuwa na fedha, watu wataendelea kukuhesabu kwa sababu ya moyo wako na utu wako.

Hitimisho

Usijenge tu mtandao wa watu wa kukusaidia, bali jenga mtandao wa watu unaowasaidia na wao pia.
Usiwe tu yule anayejua kupiga simu akiishiwa, bali pia uwe mmoja wa wale wanaoweza kupigiwa simu.

Kwa sababu mwisho wa siku, maisha si kuwa na watu wa kukusaidia pekee, bali pia wewe mwenyewe kuwa msaada kwa watu wengine.

PATA KITABU KIZURI SANA ‘”USIISHIE NJIANI” BOFYA


Discover more from Jacob Mushi

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading