Habari za leo rafiki yangu mpendwa ni furaha yangu kuona wewe ni mzima na umeweza kusoma ujumbe huu leo. Karibu sana. Katika maisha jambo linaloleta furaha mara nyingi hua ni pale unapokamilisha jambo ulilolianza. Umeweka malengo yako makubwa na ukaweza kuyafanikisha yote lazima uwe na furaha. Lakini haitakiwi uishie kwenye kufurahi tu kwa maana safari…
Sifa za watu waliofanikiwa. (1)
Kama tunavyofahamu kwamba kila kitu kilichopo ndani ya maisha ya mtu ni matokeo ya vitu alivyokua akivifanya huko nyuma, yaani kama una afya mbovu, kuna uzembe ulifanya labda hukula chakula bora, hufanyi mazoezi n.k. hivyo hivyo kwenye upande wa kifedha kama kwa sasa una tatizo la pesa ni matokeo ya uzembe ulioufanya muda uliopita. Tuankwenda…
Ona Kila unachokutana nacho kama fursa.
Tanakutana na vitu vingi sana katika maisha yetu ya kila siku, tunakutana na changamoto mbali mbali kwenye kila tunachokifanya. Watu wengi wanapopitia matatizo wanaishia kulalamika na kulaumu mwisho wa siku matatizo ndio yanakua mengi Zaidi. Leo ningependa tujaribu kubadili mtazamo wetu juu ya kila kitu tunachokutana nacho kiwe kizuri au kibaya jaribu kukiangalia kama fursa.…
Jinsi ya Kukuza Biashara yako.
Habari za Jumapili ndugu msomaji wetu. Leo tutakwenda kuona ni jinsi gani unavyoweza kutengeneza wateja kwenye mtandao wako wa blog au mitandao ya kijamii. Kama kawaida tumeshasema kwenye hii mitandao imebeba watu wa kila aina watu wa rika zote ni wewe tu ujue unawezaje kuwafikishia huduma/bidhaa yako. Hapa tutakwenda kuona njia mbalimbali:1. Toa maelezo jinsi…
Kukubaliwa na Kupingwa
Mara nyingi tumekua tukifurahi sana pale tunapowaeleza watu juu ya vitu tunavyoviwaza kama binadamu hua anapata hamasa pale anapomueleza kitu mtu na akakikubali bila kukipinga. Sio vibaya kupenda hivyo lakini kwenye ujasiriamali na mawazo ya biashara iko tofauti kidogo. Wazo lako la biashara kila mtu akilikubali na akakuambia kua inawezekana na utafanikiwa wewe kama mjasiriamali…
Kila Jambo na wakati wake.
Mwisho wa kila tunachokipigania hapa duniani ni kifo, watu wengi wanafikiri kuna siku itafika sasa aanze kupumzika na kufurahia maisha ukweli ni kwamba usipofurahia maisha sasa hivi utajikuta muda umeshakwenda na vitu ambavyo ulitakiwa ufanye wakati fulani muda wake umepita. Tunaambiwa kila jambo na wakati wake wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, chochote unachokipanda…
Kuku, Kunguru na Tai.
Ukiona tai na kuku wapo pamoja wanatafuta chakula ujue tayari tai ameshapoteza mwelekeo. Mwanamafanikio mwenzangu ni kwamba kuku hana msaada wowote kwako juu ya kupaa kwako juu ya kwenda juu zaidi. Wewe kama mtu unaetaka kufika mbali unaetaka kupaa juu kama tai tafuta tai wenzako kuku atafundisha mbinu za kukaa hapa hapa chini, kuku atakufundisha…
Ukweli ni huu Usijidanganye.
Zichukulie pande zote ni sawa. Wakati mwingine hua tunajidanganya wenyewe kwa kukataa kuambiwa ukweli. Umeanza biashara unataka kila unaemueleza akwambie nenda kafanye ni wazo zuri sana utafanikiwa akija mwingine akakueleza changamoto utakazokutana nazo unamwona mtu yule ni mbaya na hafai. Ukweli ni kwamba kwenye chochote kizuri na chenye matokeo mazuri changamoto ni lazima huwezi kuzikwepa…