Mwaka 2020 ulikuwa wa changamoto nyingi, lakini pia ulikuwa na fursa nyingi sana kwa wale waliokuwa tayari kuchukua hatua. Wengi wetu tulikuwa tunahangaika na hofu, hatari, na kutokujua mustakabali, ila wapo waliothubutu kufanya maamuzi madogo yaliyowaletea matokeo makubwa miaka michache baadaye.
Leo nataka tukumbuke mfano rahisi wa uwekezaji ambao ulionekana mdogo, lakini ulikuwa na nguvu kubwa sana ya kubadilisha maisha.
Mwaka 2020, bei ya hisa za CRDB Bank ilikuwa kati ya TZS 150 hadi 200 kwa kila hisa.
Mwaka huu 2025, hisa hizo zimepanda hadi kufikia zaidi ya TZS 1,600 kwa kila hisa.
Fikiria mtu aliyenunua tu hisa 50,000 mwaka ule kwa wastani wa TZS 200, angekuwa ametumia TZS 10,000,000 pekee. Leo angekuwa na hisa zenye thamani ya TZS 80,000,000 — bila kufanya kazi yoyote, bila kuhangaika kila siku, bali kwa kuchukua hatua ndogo tu wakati wengi walikuwa wanaona haina maana.
Mwaka huohuo 2020, mimi na rafiki yangu tulienda kuangalia viwanja Kigamboni.
Rafiki yangu aliamua kununua kiwanja kwa TZS 6,000,000, mimi nikaona bora nisubiri.
Mwaka huu 2025, bila kujenga chochote wala kufanya chochote, amekiuza TZS 26,000,000.
Kwa miaka mitano tu, ameongeza zaidi ya TZS 20 milioni kwenye mtaji wake — kwa kufanya uamuzi mmoja mdogo tu.
Leo nataka nikuulize swali rahisi lakini lenye uzito:
Ukirudi nyuma miaka mitano iliyopita, ni fursa ngapi zilipita mbele yako na hukuchukua hatua?
Labda:
- Uliwahi kuona tangazo la ardhi ukaona “bado sina hela.”
- Ulisikia/ulijifunza kuhusu hisa ukaona “hizo si zangu.”
- Au ulipata wazo la biashara ukaahirisha kwa kusema “wakati haujafika.”
Lakini ukweli ni kwamba, muda hautasubiri.
Miaka mitano imepita kimyakimya, na sasa unayaona matokeo ya wale waliothubutu wakati huo.
Je, Umejifunza Nini?
Ukweli ni huu — mabadiliko makubwa huanza na maamuzi madogo.
Hautahitaji kuwa na milioni kumi kuanza, unachohitaji ni uamuzi wa leo.
Mwaka huu 2025 umekutana na fursa ngapi?
Je, kuna mojawapo uliyochukua hatua juu yake?
Au bado unasubiri “wakati sahihi”?
Kumbuka, mwaka 2030 hauko mbali.
Utaishi katika matokeo ya maamuzi unayoyafanya leo.
Hitimisho
Tafakari maisha yako kama safari ya fursa na maamuzi.
Kila siku inakuletea nafasi mpya ya kupanda mbegu ya mafanikio ya kesho.
Usiache hofu, mashaka, au hali ya sasa ikuzuie kuchukua hatua ndogo — maana ndogo leo inaweza kuwa kubwa sana kesho.
Anza sasa.
Miaka mitano ijayo utajishukuru.
Kama ujumbe huu umekugusa, basi utapenda zaidi kusoma kitabu changu Usiishie Njiani — kitabu kinachokusaidia kujenga uthubutu, uvumilivu, na ujasiri wa kuendelea mbele hata pale unapokutana na changamoto.
Kitabu hiki kitakusaidia:
- Kutambua fursa zilizo mbele yako.
- Kuacha kuahirisha maamuzi muhimu.
- Kujenga tabia ya uthabiti na msimamo kwenye safari ya mafanikio.
Nunua nakala yako leo kupitia:
https://jacobmushi.co.tz/product/usiishie-njiani-timiza-ndoto-yako/
Discover more from Jacob Mushi
Subscribe to get the latest posts sent to your email.

