Vile ulivyo sasa kunatokana na Imani yako juu ya vitu mbalimbali vilivyokuzunguka. Matokeo mbalimbali unayopata kwenye Maisha yako yanatokana na kile unachokiamini. Ukifanya kazi kwa bidii kuliko wengine halafu moyoni mwako unaamini matajiri ni wachawi kamwe huwezi kuwa tajiri. Lazima kwanza uanze na kuamini moyoni mwako kwanza kwamba inawezekana ndipo ukija kwenye vitendo vilete matokeo.…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 187: Bado Nafasi Ipo.
Kama Umeamka tena leo basi bado nafasi ipo. Bado nafasi ya kubadilisha pale ulipokosea tena. Usiogope wala kukata tamaa kwa lolote lile kama bado unapumua ni ujumbe kwamba unayo nafasi ya kufanya mabadiliko kwenye Maisha yako. Haijalishi umepitia mangapi ya kukuvunja moyo wako na kukurudisha nyuma kama bado hujafa yaani bado upo hai. Huo ni…
HATUA YA 186: Usiwe Mmoja Wao.
Usiwe mmoja wao wanaolalamika badala ya kuchukua hatua. Usiwe mmoja wao ambao matatizo yao wenyewe wanatafuta watu wa kuwabebesha badala ya kuyatatua. Usiwe mmoja wao ambao wanafanya mambo kwa kufuata mkumbo. Usiwe mmoja wao hao ambao wanategemea maisha yao yabadikike wakati hakuna wanachokifanya ili kuyabadili. Ndio rafiki yangu nakwambia usiwe mmoja wa hao wakatishaji…
HATUA YA 185: Vitu Ambavyo Kila Mtu Anaweza Kufanya..
Siku zote kama unafanya kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya hakiwezi kuleta mchango mkubwa kwenye maisha yako. Kama unataka matokeo ya tofauti basi achana na mambo uliyozoea kuyafanya. Watu wengi wanapenda kutoa sababu na kulalamika. Kila mtu anaweza kusema lakini ni wachache wanaochukua hatua. Kila anaweza kufanya biashara lakini sio kila mmoja anaweza kufanya biashara…
HATUA YA 184: Usipoteze Muda Wako kwenye Hiki.
Muda ni kitu cha Thamani sana, muda ndio umebeba maisha yetu. Kama utakuwa unatumia muda wako kuwasema watu kwa wanayofanya unapoteza sehemu ya maisha yako. Kama mtu amefanya vibaya njia nzuri ya kumsaidia ni kwenda kumwambia na sio kumsema pembeni. Kama mtu huyu huna uwezo wa kwenda kumweleza makosa yake na unataka kweli kumsaidia tafuta…
HATUA YA 183: Chanzo ni Nini?
Hakuna kitu kinatokea chenyewe bila ya kuwepo kisababishi. Kama sasa hivi huna pesa kuna chanzo cha wewe kukosa pesa. Ukitumia muda mwingi kulalamika kwamba huna pesa utakuwa unapoteza muda. Badala yake tumia muda huo kujua nini chanzo cha wewe kukosa pesa. Umepitia changamoto yeyote kwenye Maisha yako badala ya kuumia sana, na pia kabla hujaanza…