HATUA YA 209: Hii Ndio Siri ya Kutoingia Kwenye Madeni.

Inawezekana Umekuwa Mtumwa wa madeni na hayaishi kila siku unajikuta unatengeneza madeni mapya. Suluhisho sio kuwa na pesa nyingi bali ni kuwa na nidhamu. Kwasababu hata ukiwa na pesa nyingi kama una tabia inayokuingiza kwenye madeni utajikuta unaendelea nayo kila wakati. Usinunue kitu chochote ambacho Hukupanga. Kitu chochote unachokutana nacho njiani kiwe kizuri kiasi gani,…

HATUA YA 208: Unatumiaje Kidogo Ulichonacho?

Kabla Hujawaza kupata laki tano ya kuanzia biashara anza kuonyesha uwezo wako wa kutumia elfu hamsini. Kama ukishindwa kujua utaitumiaje elfu hamsini hata laki tano utashindwa kuitumia vizuri. Watu wengi tumekuwa tunalalamikia tatizo la mtaji  lakini tatizo sio mtaji tatizo lipo kwenye akili yako. Ili uweze kupata kile kikubwa unachokitaka jifunze kutumia kidogo kilichopo karibu…

HATUA YA 207: Maneno Unayotakiwa KUJISEMESHA MWENYEWE UNAPOAMKA ASUBUHI

Kujisemesha mwenyewe ni njia nzuri sana ambayo unaweza kuitumia kutengeneza siku ambayo ni bora sana. Vile vile kwa kujisemesha mwenyewe kutakuasaidia USIISHIE NJIANI kwenye lile jambo uliloamua kulifanyia kazi. KUJISEMESHA MWENYEWE ni tiba ya akili na moyo wako hasa pale unapokuwa umeanza kupitia magumu katika kuitimiza ndoto yako. Unapopitia hali mbaya labda ni hasara kwenye…

HATUA YA 202: Ondoka Nyumbani.

Sehemu uliyoizoea ndio inafanya uwe na hali uliyonayo sasa hivi. Kama hapo ulipo unapata kila unachokitaka jiulize je utaendelea kupata unachokitaka kwa muda gani? Kama ukiona hakuna  muda mrefu hatua unayopaswa kuchukua ni kuondoka. Nyumbani kwako kunaweza kuwa ni kazini kwako pamoja na mshahara unaopokea. Inawezekana unadanganyika na mshahara unaopokea ukafikiri maisha yatakuwa hivyo siku…

HATUA YA 201: Ukitaka Kutumia Zaidi..

Kanuni ya Umaskini ni kutumia Zaidi ya unachozalisha. Kama unataka kubakia kuwa maskini endelea kuwa na matumizi makubwa kupita uwezo wako wa kuzalisha. Kama wewe ni mkulima ukizoea kula Zaidi ya unachozalisha mwisho wa siku utakula na mbegu inayokuzalishia. Kama wewe ni mfanyabiashara ukizoea kutumia Zaidi ya unachopata utaanza kula mtaji. Kanuni ya mafanikio inasema…

HATUA YA 196: Kuna Mahali Ulisababisha.

Mambo mabaya yote yanayotokea kwenye Maisha yako sio kwa bahati mbaya kuna mahali uliyasababisha yakatokea. Badala ya wewe kuchukua muda mwingi kulaumu na kulalamika jiangalie kwa upande wako unahusikaje kusababisha. Tuchukue mfano rahisi watu wawili wanagombana hadi kutaka kupigana, ukikaa na mmoja wapo ukamuuliza ilikuaje ataanza kumtupia lawama mwenzake. Lakini ukweli hadi wakafikia kugombana yeye…

HATUA YA 195: Kizazi cha Kuona Kwanza na Kuamini.

Tupo kwenye kipindi ambacho watu wake hwaamini tena mpaka waone. Kizazi ambacho hakiamini matendo ya Imani mpaka kione kwa macho ya damu na nyama. Tuna watu wengi sana ambao hawawezi kuamini chochote unachowaambia bila ya kuona ishara ya papo kwa papo. Kama huwezi kujenga Imani kwanza ndipo uone matokeo utaishia kudanganywa kwenye mambo mengi ya…

HATUA YA 193: Ukitaka Kuaminika…

Ukitaka kuaminika usiwe mtu wa kubadilika badilika kutokana na mazingira uliyopo au unapokuwa na watu wa aina Fulani. Ukitaka kuaminika kuwa wewe siku zote. Ukitaka kuaminika kuwa mtu ambaye unatabirika yaani watu wakikuacha mahali wanaamini hutabadili tabia. Unayafahamu maji? Maji ukiyaweka kwenye ndoo yatakaa na yatabeba umbo la ndoo. Vilevile maji ukiyaweka kwenye mfuko yatakaa…