Watanzania wengi ni wavivu sana kusoma, kabla hujaamini picha ya kichwa cha habari inayosambazwa jaribu kutafuta habari nzima uisome na uelewe.
Vichwa vingi vya habari huandikwa kwa namna ya kuvuta wasomaji na bahati mbaya sana wengi wenu huishia kusoma kichwa tu na kufikia hitimisho.
Usiwe mwepesi pia kuamini kila kilichoandikwa kwasababu kwenye ulimwengu wa sasa hivi kila mtu anaweza kuwa na tovuti yake na akaandika mawazo yake.
Hakikisha unachokiamini umekipata kwenye chanzo kinachoamini au umethibitisha kwa kufuatilia sehemu tofauti tofauti.
Kwa kifupi Usikubali Kuwa Mjinga, Usikubali kulishwa ujinga, Tafuta Taarifa sahihi. Tafuta taarifa za Ukweli na Uhakika.
By Jacob Mushi
Discover more from Jacob Mushi
Subscribe to get the latest posts sent to your email.


Asante sana